Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba amesema kuwa anatarajia kuingiza sokoni bidhaa zake kutoka katika brand yake ya ‘AK’ pamoja na ‘King Kiba’.

Kiba amesema kuwa hiyo ni mipango mizito na hatarajii kuifanya kiholela kwani hata mwanzo alitoa baadhi ya bidhaa kama promotion ila sasa bidhaa kamili zinakuja.

Mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo Aje amesema kuwa anashukuru kwassa baadhi ya bidhaa zake watu wanavaa kutoka kwenye brand ya AK ila sasa watarajie kazi nyingine kutoka brand yake ya King Kiba.

Alikiba ametaja baadhi ya bidhaa hizo ni jeans, mawani pamoja na Energy drink ambapo zitatoka hivi karibuni.

Mkali huyo anafuata nyayo za mkali mwenzake Diamond ambaye mwezi uliopita amezindua bidhaa yake ya Perfume ijulikanayo kama Chibu Perfume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *