Mkali wa nyimbo ya ‘Aje’ Alikiba anatarajiwa kufanya show katika mji wa Mombasa nchini Kenya ijulikanayo kama “Mombasa Rocks Music Festival” siku ya Oktoba 8 mwaka huu.

Katika show hiyo Alikba ataungana na wanamuziki nyota kama Chris Brown kutoka nchini Marekani pamoja na Wizkd kutoka nchini Nigeria ambao pia watatoa burudani kwenye tamasha hilo litakalofanyika Mombasa.

Tamasha hilo litafanyika katika ukumbi wa Mombasa Golf Club kwenye mji wa Mombasa nchini Kenya ambapo Alikba amechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika tamasha hilo kubwa litakalofanyika Okota 8 mwaka huu.

Chris Brown na Wizkid
Chris Brown na Wizkid

Mbali na show hiyo ya Mombasa Alikiba pia anatarajia kufanya show katika utoaji wa tuzo za MTV MAMA zitakazofanyika katika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini akiwa pamoja na nyota mwenzie kutoka Tanzania Diamond Platnumz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *