Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba amewashuru mashabiki wake baada ya wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ kufikisha views zaidi milioni nne ndani ya siku 10.

Wimbo huo ambao umeachiwa Agosti 25 mwaka huu umekuwa gumzo nchini kutokana na ubora wake na mpaka kupelekea kufikisha watazamaji milioni nne ndani ya siku 10 jambo ambalo si la kawaida kwa wasanii wa Tanzania.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Alikiba amewashakuru mashabiki zake kwa kuendelea kuifanya ngoma hiyo kushika nafasi ya kwanza katika video ambazo zinafanya vizuri Tanzania toka ilipotoka Agosti 25, 2017.

Alikiba ameandika “Seduce Me imefikisha watazamaji milioni 4 ndani ya siku 10 na bado inaendelea kushika nafasi ya kwanza kwa video zinazo ‘trend’ Tanzania, nawakubali wote na kuwathamini lakini pia nawapenda sana Tanzania”.

Seduce Me ni wimbo ambao umemrudisha tena Kiba baada ya kukaa muda mrefu bila ya kuachia wimbo toka alipoachia ‘Aje’ ambayo pia ilifanya vizuri.

vevo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *