Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba jana ametangazwa rasmi kuwa mmoja kati ya wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000 ambayo anafanya nayo kazi.

Alikiba amefanya kazi na kampuni hiyo kwa miaka sita toka ajiunge nayo kwa kusimamiwa na kazi zake za muziki.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Rockstar4000, Muimbaji huyo atakuwa mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo, pia atakuwa Director of Music and Talents.

Taarifa hiyo imesema kuwa “Usiku wa jana King Kiba ametangazwa rasmi kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television,”.

Pia taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa “Alikiba kwa sasa anakuwa sehemu ya wasanii waliochini ya Rockstar4000 pia anakuwa Director of Music n Talents,”

Rockstar Television inajishughulisha na utengenezaji wa vipindi vya mastara tofauti kutoka nchi mbalimbali na kuvisambaza katika vituo vya Television vya kimataifa.

Kampuni hiyo kwasasa nchini Tanzania inamsimamia Baraka The Prince, Lady Jay Dee pamoja na yeye mwenyewe Alikiba.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *