Mkali wa Bongo fleva, Alikiba ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwenye mechi ya Hisani kwa ajili ya kusaidia mama wajawazito ujilikanao kama ‘Dorah Foundation’ iliofanyika jana nchini Uganda.

Mechi hiyo ilihusisha mastaa kibao nchini humo akiwamo Emanuel Okwi aliyecheza timu moja na Alikiba ambapo timu yao ilikuwa inaitwa ‘The Celebrity White Team’ na wakafanikiwa kuibuka na ushindi wa 4-1.

okwi

Alikiba alitoa mchango mkubwa sana kwa upande wa timu yake mpaka kupelekea kupata tuzo hiyo ya mchezaji bora ‘The Best Celebrity Player Award’ katika mechi hiyo.

Alikiba ni mwanamuziki na pia mwanasoka anayecheza mchezo huo kwa ustadi mkubwa mpaka kupelekea kupata tuzo ya mchezaji bora wa mechi licha ya kuwepo kwa wachezaji wakubwa na Emanuel Okwi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *