Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba jana amesherehekea siku yake ya kuzaliwa katika mbuga ya wanyama ya Serengeti baada ya kutimiza miaka 30.
Kiba amezaliwa Novemba 29, 1986 aliamua kusherehekea siku hiyo tofauti na mastaa wenzake baada ya kufanya sherehe hiyo katika Hifadhi hiyo Serengeti.
Mkali huyo ameweka baadhi ya picha za sherehe hiyo kupitia akaunti yake ya Instagran akiwa Sayari Camp, Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti akiwa na staa mwenzake Baraka Da Prince.
Wengine waliohudhuria sherehe hiyo ya Kiba ni meneja wake Seven Mosha pamoja na wananchi wengine walioshiriki hafla hiyo.