Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba kupitia akaunti yake ya Instagram amempongeza waziri mpya wa fedha wa Afrika Kusini, Malus Gigaba kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.

Malus Gigada amechaguliwa na Rais wa Afrika Kusini kushika wadhifa wa waziri wa fedha baada ya kutimuliwa kwa Pravin Gordhan.

Alikiba ameandika maneno ya pongezi kwa waziri huyo pamoja na picha akiwa pamoja wakati alipokuwa na ziara ya kimuziki nchini Afrika mwezi wa pili.

Kupitia akaunti hiyo ya Instagram Kiba ameandika “Honorable minister Gigaba @malusi_gigaba, it’s such an honour to be an Ambassador under one of the campaigns you started for Africa as Minister of Home Affairs: Stop child Trafficking.

Pia ameongeza kwa kuandika “I want to thank you for the opportunity and congratulate you in your new role as the Minister of Finance For South Africa, Stay blessed”.

Mwanamzuki huyo kwasasa yupo nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki ambapo anatoa show katika miji tofauti nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *