Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amekanusha tuhuma za kuiba wimbo mpya ‘Seduce Me ‘.

Alikiba amesema kuwa katu kitu kama hicho hakitaweza kikatokea kwenye maisha yake na kuwatoa hofu mashabiki zake wasiumizwe na maneno kwani anajiamini.

Mwanamuziki huyo ameamua kukana tuhuma hizo baada ya maneno mitandaoni ya kwamba wimbo wa ‘Seduce Me’ uliotengenezewa na mtayarishaji Man Water umefanyiwa  ‘copy’ kutoka kwenye wimbo ulioimbwa na kwa lafudhi ya kiharabu .

Pamoja na hayo Alikiba amewasihi mashabiki zake wasiwe na hofu kwani hawezi kukaa kimya kwa muda mrefu kwani mwaka huu amepanga kuwafurahisha na pindi watakapokuwa wanataka ngoma mpya wasisite kumtaarifu ili aachie kazi nyingine mpya.

Kwa sasa Alikiba anasumbua na ngoma inayokwenda kwa jina la ‘Seduce Me’ iliyotoka Agosti 25 ambapo mpaka sasa inawatazamaji zaidi ya milioni 4 katika mtandao wa YouTube kupitia account yake ya ‘Vevo’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *