Mkali wa ‘Aje’ Alikiba amekanusha kufanya kolabo na mwamuziki nyota wa Marekani Justin Bieber.

Kauli hiyo Alikiba imekuja baada ya kuenea taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mkali huyo ana mpango wa kufanya ngoma na Jstine Bieber.

Alikiba amesema kuwa taarifa za kwamba ana mpango wa kufanya kolabo na mwanamuziki huyo zilianzishwa na mashabiki wake wa muziki.

hqdefault

Pia muimbaji huyo alidai hana mpango wakufanya kolabo na Wizkid kwa sasa lakini ukifika muda na akipata nafasi anaweza kufanya hivyo kutokana na kuwa katika lebo moja ya Sony Music.

Kiba kwasasa yupo katika mji wa Las Vegasi nchini Marekani alipokwenda kufanya show kutokana na ratiba yake ya kimuziki nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *