Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva, Alikiba amewapagawisha mashabiki wa muziki huo waliofurika kwenye show ya Mombasa Rocks Music Festival usiku wa kuamkia leo mjini Mombasa.

Mashabiki walijitokeza kwenye tamasha hilo wameonekana wakimshangilia Alikiba ikionesha jinsi gani staa huyo anavyokubalika nchini Kenya hususani katika mji wa Mombasa lilipofanyika tamasha hilo.

Alikiba: Akitumbuiza wakati wa show hiyo jijini Mombasa.
Alikiba: Akitumbuiza wakati wa show hiyo jijini Mombasa.

Mbali na Alikiba wengine waliotumbuiza kwenye tamasha hilo alikuwemo Vanessa Mdee kutoka Tanzania naye alilishambuliaji jukwaa vya kutosha kutokana na vibao vyake kufanya vizuri katika mji wa Mombasa.

Wasanii wengine waliotoa burudani walikuwa ni Chris Brown kutoka nchini Marekani pamoja na Wizkid kutokea pande za Nigeria.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *