Mkali wa Bongo fleva anayetamba na wimbo wake ‘Aje’ Alikiba amesema kuwa akupendezewa na kilichotokea kwenye Tamasha la Mombasa baada ya kukatizwa kwa show yake.

Alikiba ametumbuiza nyimbo mbili tu kabla ya mic aliyokuwa anaitumia kuonekana kuzimwa na kumlazimu kuondoka jukwaani kabla ya mwisho wa show yake.

Alikiba amedai kuwa amefanyiwa hujuma kwenye show hiyo kutoakana na kitendo cha mic hiyo kuzimwa kila muda wakati mashabiki wake walikuwa bado hawajafaidika na show yake..

Kiba amesem kila mtu alikuwa na makubaliano yake kwenye show hiyo wakati mkataba wa Chris Brown unasemekana ni kwamba alikuwa anataka kuondoka muda mchache na dakika alizokuwa amepewa ni 80.

Mkali huyo amesema kuwa  alimuona meneja wa Diamond alikuwepo pale huku akisema amefuata nini backstage wakati yeye anaperform, yeye anahusika kama nani? Haileti picha nzuri.

Kiba aliendelea kusema kwasababu hata kama watu wanafikiria kwamba of course hatuna beef lakini sasa umefuata nini na vitu kama hivyo vinahappen, wewe unafikiria watu watafikiria nini? Kitu gani kimemfanya aje?

Kuna watu wengi waliokaa kwenye VIP unaweza ukaangalia show, kuja kwenye show, kaa kwenye VIP, angalia show. But alikuwa anafanya nini backstage wakati mimi naperform?” amehoji msanii huyo.

Hata hivyo anasema hawezi kumfikiria moja kwa moja kuwa meneja huyo wa Diamond alihusika kwenye tukio hilo, japo hakuubariki uwepo wake nyuma ya jukwaa la tamasha hilo.

Kiba alimalizia kwa kusema “Sijajua mic imekatwa kwasababu Chris Brown alitakiwa kupanda au ni nini lakini nimekuwa surprised kwasababu unajua niko na fanbase kuwa na watu walikuwa wanaexpect hata before sijapanda walikuwa wanataka mimi niperform, wananiita ‘Ali Ali, vipi unakuwaje.’ Nikaingia, sijamaliza kuperform wamekataa mic, I think wameelewa kitu gani kinaendelea sababu it was not my fault.”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *