Mkali wa ‘Aje’ Alikiba amefunguka na kusema kuwa msanii Baraka The Prince hakumuangusha kabisa kwenye wimbo wao wa pamoja ‘Nisamehe’ ambao video yake imefanyika nchini Afrika Kusini.

Alikiba amesema kuwa kwake yeye ilikuwa rahisi sana kukubaliana na wazo la Baraka kwa kuwa msanii huyo kwanza anakipaji kikubwa lakini pia ni watu ambao wanaendana katika kazi.

Alikiba amesema Baraka The Prince anapita sehemu alizokanyanga yeye ndiyo maana imekuwa rahisi wao kufanya kazi ya pamoja ambayo mwisho wa siku imeweza kuwa nzuri na kila mmoja amepita vizuri.

Baraka The Prince imekuwa raisi kufanya kazi na AliKiba kutokana na wote kusimamiwa na kampuni moja ya Rockstaa4000.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *