Mkali wa Bongo Fleva, Alikiba amesema kuwa katika kazi yake ya muziki hakuna mtu anayeshindana naye.

Alikiba amedai ila kama kuna watu wanataka kushindana na yeye basi atawaacha na kuendelea na mambo yake.

Mwanamuziki huyo amesema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa katika njia yake ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi.

Kiba amesema kuwa anaamini akiwapa nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya hasa zaidi katika muziki wake.

Pia amesema kuwa yeye haangalii ushindani na wala hashindani na mtu yeyeto kwenye muziki wake ndiyo mana anafanikiwa kwenye kazi yake hiyo.

Kiba anahusishwa kushindani na mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz lakini yeye amepinga hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *