Mwanamuziki nyota wa Marekani, Alicia Keys ametangaza kuachia albamu yake ya sita itakayoitwa kwa jina ‘Here’ ifikapo Novemba 4 mwaka huu.

Alicia Keys alitangaza ujio wa albamu hiyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter baada ya kuandika ujumbe unaosomeka, “My new album: HERE. Out 11/4. Pre-order to receive my new song Blended Family (What You Do For Love) today

Albamu hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 16 ikiwemo ‘In Common’, ‘Blended Family (What You Do For Love’, na nyingine kibao.

Kwa mara ya mwisho Alicia Keys kuachia albam ilikuwa mwaka 2012 ambapo albamu hiyo ilijulikana kwa jina la ‘Girl On Fire’.

Ujio wa albamu hiyo utaweza kuvunja ukimya wa mwanamuziki huyo kutokana na kukaa kimya kwa miaka mingi bila ya kuachia albamu mpya bila shaka mashabiki wake wapo tayari kuipokea albamu hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *