Mwanamuziki nyota kutoka Marekani, Alicia Keys amefunguka kuhusu kujiamini kwake kutembea kwenye shughuli kubwa za muziki bila kujipaka vipodozi usoni mwake.

Alicia Keys amesema ilichukua muda mrefu sana kusafisha ngozi yake ili kuweza kukaa mbele za watu bila kipodozi chochote usoni mwake.

Keys amesema siri yake ilikuwa kupunguza mafuta na cream alizokuwa akinywa kabla hanajapa ujauzito na akazidisha kiasi cha maji anachokunywa kwa siku ndio maana ngozi yake ikawa safi.

Kwa sasa Alicia Keys anatembea bila kujipaka kipodozi chochote kwenye Red Carpet na hata kwenye kiti chake cha ujaji wa shindano la vipaji la The Voice.

Alicia Keys amekuwa tofauti na wasanii wengine ambao hawawezi kwenda kwenye shughuli yoyote bila ya kupata make up.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *