Mbunge wa Kilombero (Chadema) Peter Lijualikali  baada ya kuachiwa huru na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, ametoa ya moyoni na kusema kuwa alichofanyiwa ni uonevu.

Ameyasema hayo leo baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, kukamilisha taratibu za kumtoa gerezani.

Lijualikali amefutiwa mashtaka yake jana na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam baada ya kukaa jela kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa masharti ya faini.

Mbunge huyo alihukumiwa kwenda jela miezi sita bila faini baada ya kukutwa na hatia ya kuwafanyia fujo polisi wakati wa Uchaguzi Mkuu  mwaka 2015.

Lijuakali na dereva wake, John Bikasa walikutwa na hatia ya kukata utepe wa polisi na kuwafanyia fujo jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *