Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametoa maoni yake kuhusu uwezekano wa Barcelona kujiunga na ligi kuu ya Uingereza kama watajitenga na Uhispania.

Wenger amekiri kwamba kama klabu hiyo itajiunga na kwenye ligi ya Uingereza mambo yatakuwa magumu zaidi kutokana na ubora wa ligi hiyo.

Kutokana na hali ya kisiasa huko Catalonia, kulikuwa na uvumi kuhusu kule ambako Barcelona itacheza iwapo italazimika kuondoka la Liga.

Wenger aliulizwa kuhusu uwezekano huo wa kucheza nchini Uingereza na ni nini angefanya iwapo hilo lingefanyika.

Na alipoulizwa iwapo angeikaribisha katika ligi ya Uingereza, raia huyo wa Ufaransa alisema ingekuwa muhimu iwapo wangeangazia klabu nyengine za nyumbani iwapo wangetaka kupanua ligi hiyo.

Wenger amesema kuwa ”Tuna vilabu vya kutosha takriban 20 lakini iwapo unataka kuongeza vilabu hivyo hadi 24 ni vyema kuvialika vilabu vya Uskochi kabla ya kuelekea Uhispania”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *