Promota wa ngumi nchini Kaike Siraju amemshambulia kwa maneno bondia Francis Cheka baada ya kutopanda ulingoni Jumapili hii katika pambano lake dhidi ya bondia Abdallah Pazi (Dullah Mbabe).

Kaike ambaye ndiye aliyekuwa Promota wa pambano hilo, ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo kilichofanywa na Cheka, huku akisisitiza kuwa Cheka anatakiwa kupimwa akili kwa madai kuwa kitendo alichokifanya hakiwezi kufanywa na binadamu mwenye akili timamu.

Akizungumzia madai ya Cheka kwamba alikuwa hajalipwa, Siraju amesema tayari alikuwa amekwishatoa pesa ya utangulizi shilingi milioni 4 na kwa mujibu wa taratibu za mapambano, alipaswa kumaliziwa pesa yake muda ambao anapanda ulingoni, lakini Cheka aligoma tangu mapema kucheza pambano hilo licha ya kuwa walikuwa wamekwisha kubaliana kila kitu.

Kuhusiana na madai kuwa Cheka alikuwa akimdai pesa, Kaike amemtaka Cheka kujitokeza hadharani na kusema ukweli kama kuna hela nyingine anayomdai na aseme ni kiasi gani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *