Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda amesema ameguswa na hisia za Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Ponda amesema hayo leo akizungumzia safari yake ya Nairobi nchini Kenya alikokwenda kumjulia hali Lissu hivi karibuni.

Pia amesema kuwa “Tulipokuwa tunabadilisha mawazo, niliguswa na hisia kubwa, badala ya mimi kumpa matumaini yeye ndiye alinipa matumaini,”.

Amesema madhumuni ya safari yake yalikuwa kumjulia hali Lissu, kumwombea dua, kumjengea matumaini ya afya na kujenga mazingira mapana yanayotosha kulizungumza jambo lililomfika.

Lissu anapata matibabu katika Hospitali ya Nairobi baada ya kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Sheikh Ponda amesema Lissu alimweleza hivi karibuni atarudi katika harakati na ataanzia alipoishia.

“Amehimiza mshikamano na alionyesha ana matumaini na Watanzania kwa harakati wanazozifanya,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *