Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuapisha Kamanda Simon Sirro kuwa mkuu wa mpya wa jeshi la Polisi nchini, aliyekuwa mkuu wa Jeshi hilo Ernest Mangu afunguka uteuzi huo.

Mangu amewataka wananchi pamoja na jeshi la Polisi nchini kumpa ushirikiano kamanda Sirro ili kufanikisha kazi aliyopewa na Rais Magufuli baada ya kuteuliwa hapo jana.

Kauli hiyo ameitoa leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kuapishwa kwa kamanda Sirro.

Mangu amesema kuwa anamfahamu Sirro ni mchapakazi kwa hiyo wananchi wampe ushirikiano katika kazi yake ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na amani  kwa kutatua vitendo vya kiharifu.

Kuhusu mauaji ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji, Mangu amesema kuwa anaamini kamanda Sirro atatatua tatizo hilo kutokana ana mfahamu kuwa ni mchapakazi kinachotakiwa wananchi na jeshi la Polisi kumuunga mkono kamanda huyo mpya.

Mangu atapangiwa kazi nyingine hapo baadae baada ya uteuzi wake kutenguliwa jana na Rais Magufuli na cheo chake kurithiwa na kamanda Sirro aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *