Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva kutoka ‘Combination Sound’ Man Water amesema kuwa sababu za msanii wake 20% kushindwa kurudi kwenye game kama awali ni kutokana na kushindwa kutumiza malengo yao baada ya kupata matatizo ya kifamilia.

Man Water amesema kuwa sababu kubwa ambayo imepelekea msanii 20% kushindwa kurudi kama ambavyo watu walikuwa wakitarajia kutoakana na uongozi wake mpya.

Mtayarishaji huyo ambaye pia ni muimbaji amesema kuwa managementi hiyo imeshindwa  kutimiza mipango yao kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo 20% alikuwa akikabiliana nayo lakini pia mipango yao haikuwa mizuri jambo ambalo hawataki litokee tena.

Man Walter aliongeza kwa kusema kuwa walikuwa na mipango ila ilishindwa kutimia, pia walikuwa na mipango ya kufanya video na walituangalia video ingekuaje, bajeti ipoje yaani kulikuwa na mambo mengi sana wakati huo huo 20% alifiwa na dada yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *