Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amempongeza Lissu kwa ushindi mkubwa alioupata kwenye uchaguzi wa chama cha wanasheria nchini (TLS).

Lowassa amesema ushindi wa Lissu ni joto la moto mkubwa wa mabadiliko uliotuama ndani ya mioyo ya Watanzania.

Uchaguzi ule naweza kusema ulikuwa kama kura ya maoni kwa wanasheria dhidi ya Serikali jinsi inavyoheshimu demokrasia ya umma na utawala wa sheria,’’.

Tundu Lissu ameshinda urais wa Chama Cha Wanasheria nchini (TLS) kwenye uchaguzi uliofanyika jana jijini Arusha.

Tundu Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema ameibuka mshindi kwa asilimia 88 baada ya kupata kura 1411 na kuwaacha wapinzani wake kwa mbali sana.

Mbali na nafasi hiyo ya Urais pia kulikuwa na uchaguzi wa wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *