Muigizaji wa bongo movie, Aunt Ezekiel amesema kuwa hana mpango wa kumuinginza mpenzi wake Mose Iyobo kwenye tasnia ya bongo movie.

Aunt amesema kuwa anapenda anavyokuwa anacheza na ajawahi kuwaza kumtoa kwenye kipaji chake na kumuingiza kwenye movie  hata kama akitaka kuacha kipaji chake ni bora ajiingize kwenye biashara lakini siyo kujiingiza kwenye movie kwani siyo kipaji chake.

Aunt amesema yeye hakuvutwa na mtu kuingia kwenye uigizaji na ndiyo maana alifanikiwa kupitia bongo v movie  hivyo yeye atabaki kuwa muigizaji na Iyobo atabaki na mauno yake.

Muigizaji huyo ameongeza kusema kuwa alivutiwa na Mose Iyobo kutokana na kazi yake hivyo hawezi kumtoa kwenye kazi yake hiyo.

Wapenzi hao hadi sasa wana mtoto mmoja anayeitwa Kuki ambapo mapenzi yao yameanza miaka mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *