Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameamua kutumia akaunti ya Twitter kuwajulisha kinachoendelea kuhusu ripoti ya mkuu wa mkoa, Paul Makonda baada ya kuvamia ofisi za Clouds Media.

Nape jana alifanya ziara makao makuu ya Clouds Media Group baada Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari.

Waziri Nape aliunda Tume ya uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo na kutoa saa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Makonda.

Kutokana na watu kumsumbua kwa kumpigia simu kuhusu ripoti hiyo Nape ametoa majibu kupitia akaunti yake ya Twitter.

xxxx

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *