Mwanamuziki mkongwe nchini, Stara Thomas amesema kuwa sababu ambazo zinawafanya wasanii wa kike wapotee kwenye muziki ni kuendekeza mapenzi kuliko kazi zao za sanaa.

Stara Thomas amedai wasanii wengi wanashindwa kurudi kwenye biashara ya muziki kutokana na kukata kwa mitaji ya kuweza kufanya biashara hiyo kutokana na vitendo vyao kama ulevi pamoja na kuendekeza mapenzi.

Pia amesema kuwa kuna vitu vingi vinavyopelekea mtu kushuka kimuziki kwanza ni ‘mind set’ ya mtu mwenyewe lakini unajua mwanamke kama mwanamke ikifika mahali akiendekeza sana mapenzi lazima ashuke.

Vile vile amesema kuwa wengine wanakula unga, wanakunywa pombe sanaa kwa hiyo wanashindwa kuangalia biashara yao hiyo maana muziki sasa ni biashara, mara anakuja kushtukia msingi wake wa biashara hiyo umekata.

Stara Thomas ni mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva aliyejizoela umaarufu mkubwa miaka ya nyuma kutokana na vibao vyake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *