Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Solo Thang amesema kuwa akufanya kusudi kuweka video mtandaoni ikimuonesha Chidi Benz akiwa amelewa dawa za kulevya.

Solo Thang amefunguka hao baada ya baadhi ya watu kumjia juu kwa kusambaza kipande cha video hiyo akiwa na Chidi Benz.

Mkali huyo amesema kuwa Chidi ndiye aliyemtaka amshoot video wakati walipokutana ila hakuwa na nia kama watu wengine wanavyofikiria.

Rapper huyo ameongeza kuwa watu waache kumlaumu Chidi kwa kile kilichomtokea na badala yake wanatakiwa kumpatia msaada bila ya kuchoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *