Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amesema ugomvi wa Diamond ana Alikiba haujaathiri wimbo wake hata mmoja.

Nay amesema kuwa kipimo cha ngoma zake kufika mbali ni pale anapokuwa kwenye show au mapokezi ya watu mtaani ila mambo ya mtandaoni hayaathiri chochote.

“Majibu ya wimbo unayapata kwenye show, majibu ya wimbo unayapata mtaani, mimi nafanya muziki kwa ajili ya watu wangu wa mtaani siyo watu wa kwenye mitandao” amesema.

Ameongeza kuwa nguvu yake ya mtandaoni anaijua na nguvu yake ya mtaani anaijua, hivyo majibu sahihi yanayothibitisha ukubwa wa wimbo wake ni pale anapokuwa kwenye show jinsi watu wanakuwa wanaimba na kupokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *