Mwanamuziki wa nyimbo za asili, Mrisho Mpoto ametumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea ishu ya madawa ya kulevya inayoendelea nchini baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kutaja orodha ya mastaa wanaoutumia na kuuza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mrisho Mpoto ameweka picha ikiwaonyesha vijana wamemzunguka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kwenye picha hiyo Mpoto ameandika ujumbe ufuatao “Unga unamaliza nguvu-kazi ya taifa, huu ni muonekano wa vijana wa kesho tukichelewa kushirikiana, ”.

Mpoto amesema kwamba amani haipatikani kwenye utegemezi na haiendani na vitendo vya uhalifu. Unga unapoteza nguvu-kazi na kuchochea uhalifu.

Katika ujumbe huo, Mpoto ameomba ushirikiano ili kuwanusuru vijana ambao ndiyo taifa la leo.

Kauli hiyo ya Mpoto imekuja baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwataja wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie pamoja na wamiliki wa kumbi za starehe kujihusisha na masuala ya madawa ya kulevya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *