Mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobeto ametoa siri ambayo watu wengi walikuwa hawaifahamu kuhusu mahusiano yake na Diamond.

Mobeto amesema kuwa tangu awe katika mahusiano ya kimapenzi na msanii Diamond Platinumz sasa ni takribani miaka tisa na huu unaingia mwaka wa kumi wawili hao kuwa pamoja.

Aidha ameeleza chanzo cha kumfungulia kesi mzazi mwenzake Diamond Platinumz mnamo oktoba 5 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto, amesema kuwa Diamond Platinumz ndiye aliyemshauri wafungue kesi ili kuhakikisha mtoto wake anapata haki yake ya msingi kutoka kwa baba.

Pia ameeleza kuwa sio rahisi kwa mtu uliyempenda namliyekubaliana kubeba mimba wakati wote mlikuwa pamoja kukwaruzana tu kidogo ndio iwe sababu ya kumfungulia kesi ameongeza kwa kusema labda uyo mtu ulikuwa huna mapenzi nae.

” Mwanamke ambaye anakubali kukubea mimba, mnalea wote mimba miezi tisa halafu mgombane tu kidogo akupeleke mahakamani huyo mtu awe hajawahi kukupenda, mtu ambaye nina takribani miaka tisa na sasa inaingia kumi nsiwezi kukurupuka na kusema namfungulia mashtaka” amesema Hamisa Mobetto.

Hata hivyo Hamisa amesema kuwa anatamani kuyamaliza na mzazi mwenzie Zari kwani anaamini kuwa kugombana kupo hata glasi zinagongana katika kabati, ila ana amini kuwa ipo siku watakuwa pamoja kwani tayari wanakitu kinachowaunganisha pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *