Staa wa wimbo ‘Hela’ Madee amesema kuwa kundi lao Tip Top Connection alijasambaratika kama inavyosemwa ila kila mtu anafanya kazi kimpango wake kutokana na soko la muziki lilivyo sasa.

Kwasasa kundi hilo halijatoa wimbo wa pamoja kwa muda mrefu ambaye anatamba na sasa wamekubaki kama familia ya watu waliowahi kuishi pamoja na si kufanya muziki kwa lengo la biashara.

Madee amesema sababu kubwa kutotoa kazi kama kundi ni kutokana na biashara kwani saizi kila msanii anaangalia zaidi maslahi yake kuliko kundi na inakuwa inalipa zaidi kufanya kazi kama ‘Solo Artist’ kuliko kufanya kazi kama kundi.

Mbali na hilo Madee ameweka wazi kuwa tayari kuna kazi wamefanya kama kundi wamemshirikisha Diamond Platnumz na kusema kuwa siku yoyote ile wanaweza kuiachia kwa ajili ya mashabiki zao.

Kundi la Tip Top ni miongoni mwa kundi kongwe lililoanzishwa miaka ya nyuma ambapo wasanii wengi wamepita katika kundi hilo linaloongozwa na Madee ambapo maskani ni maeneo ya Manzese.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *