Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amesema kuwa nyimbo atakayofanya Alikiba na Ommy Dimpoz lazima itakuwa bora kutokana na wasanii hao kuwa na vipaji vya hali ya juu.

Lulu amesema kuwa wakali hao wa bongo fleva wamekuwa wakifanya vyema kila walipokutana na kutengeneza kazi nzuri ambazo zinapendwa na watu.

kibaommy

Mkali huyo amesema sababu kubwa kuipenda video ya ‘Kajiandae’ kwanza namna wasanii pamoja na dancers walivyoweza kuvaa vizuri, lakini pia mwanamke aliyetumika kama video queen alikuwa na muonekano mzuri wenye kuvutia na kuleta utofauti.

Muigizaji huyo amejizolea umaarufu kupitia fani yake ya uigizaji katika sekta ya Bongo movie kutokana na movie zake alizowahi kuigiza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *