Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amemkiangia kifua Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady baada ya watu kumshtumu kutokana na kusambaa picha zake akila bata siku chache tangu afiwe na Mama yake mzazi.
Watu wamekuwa wakimtupia lawama Zari kutokana na kutokujali msiba wa mama yake mzazi ambaye toka afariki hata mwezi haujafika lakini bidada huyo ameonekana akila bata maeneo ya Mombasa akiwa na Diamond.
Harmonize ambaye naye alikuwepo katika bata hilo Mombasa nchini Kenya, amesema mtu akipata matatizo halafu akapelekwa sehemu nzuri kwa ajili ya kufurahi ni kitu cha kumshukuru Mwenyenzi Mungu.
“Kwa sababu haikuwa rahisi, unajua kufiwa na mazazi sio kitu kidogo. Tumefika (Mombasa) tumemkuta yupo fresh, yaani kasharidhika na matokeo kwa sababu anajua hakuna binadamu atakuja kuishi milele,”
Harmonize amesema kuwa “Kwanza ukiona mtu anazungumza hiyo ujue haijui dini, kwa sababu dini imeandika kila mtu atakufa, kifo ni kitu cha lazima, ukiwa unaijua dini huwezi kuhofia suala la kifo. Mtu kafariki ni lazima uumie ila ni lazima maisha mengine yaendelee kwa sababu hata ukae ndani miaka sita hawezi kurudi,”.