Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka sababu ambazo watu wamekuwa wakidai haendani na aliyekuwa mpenzi wake, Jacqueline Wolper.

Harmonize amesema kuwa watu wamekuwa wakisema hawaendani na Wolper kwa sababu yeye alianza kuwa staa kabla yake na pia Wolper ana kipato kikubwa.

Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema kuwa watu walikuwa wanaongelea sana kuhusu mahusiano yao ambapo wamedumu kwa muda mchache ambapo kwasasa wameachana.

Kwa upande mwingine Harmonize amesema kuwa “Nimetengeneza ngoma nyingi sana huenda ningeweza kuziachia kila mwezi lakini lazima tupeane  mimi na wasanii wenzangu wa WCB. (Rich Mavoko, Queen Darlin na Rayvany).

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda na jina la ‘Niambie’ ambao ameutoa wiki chache zilizopita.

Kwenye wimbo huo Harmonize amethibitisha kuwa nyimbo hiyo ameutunga alipokuwa na mpenzi wake huyo na aliutunga kwa ajili ya Wolper.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *