Mkali wa hip hop Bongo, Fareed Kubanda A.K.A Fid Q amefunguka kwa kusema kuwa  anashangazwa na baadhi ya watu wanaomuandika vibaya katika mitandao ya kijamii kuwa ana ‘bifu’ na Joh Makini.

Fid amesema hajawahi hata kuwaza kugombana na rapa huyo mwenye kutoka kundi la Weusi ambapo anatamba na wimbo unaokwenda jina la ‘Waya’.

Pia amesema kuwa “Unajua hata mimi nilikuwa nazipokea tu hizo ‘story’ kama wanavyopokea watu wengine maana sijawahi kuwa na shida na jamaa, kawaida ya wabongo huwa tunatafuta ‘challenger’ kama mtu mpya akiingia kwenye game so Joh alitumiwa kama ‘challenger’ wangu maana mimi nafanya vizuri tangu back then”.

Mbali na hilo mkali huyo amesema njia ya muziki na kibinadamu hana kinyongo wala ugomvi pia aliendelea kusisitizia kuwa yeye ndiye aliyemuunganisha Joh katika ‘project ya nje kwenda kufanya kazi japokuwa muhusika mwenyewe atakuwa hatambui hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *