Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amemtaka Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuikosoa Serikali yake pasipo kuvunja sheria za nchi.

Hayo ameyasema Ikulu mjini Unguja wakati akiadhimisha mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani kupitia uchaguzi wa marudio wa Machi 20 mwaka jana.

Dk Shein amesema Maalim Seif ana uhuru wa kusema akitakacho wakati wowote, lakini asitumie lugha za matusi.

Dk Shein amesema kuna maneno mengi yamekuwa yakisemwa mitaani juu ya kuwapo kwa Serikali nyingine badala ya anayoiongoza, kauli alizosema hazina mashiko.

Pia amesema njia ya kupata Serikali ni mbili tu duniani kote, ya kupigwa kura au kufanyika mapinduzi kwa upande unaoona umedhulumiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *