Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amempongeza mwanamuziki chipukizi, Harmorapa kutokana na kujituma kwake kwenye kazi yake ya muziki.

Diamond amesema kuwa Harmorapa mpaka kufikia hapo alipo amefanya kazi kubwa sana licha ya watu kuona kama amepata nafasi hiyo kirahisi.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kila mtu anatafuta njia yake ya kujipatia ridhiki kutoka na kazi yake hiyo kwa hiyo ana budi kumuunga mkono kwenye kazi yake kwasababu nae anatafuta ridhiki.

Harmorapa
Harmorapa

Pia Diamond amemtaka Harmorapa kufanya kazi nzuri ili haweze kuonesha kipaji chake kwa mashabiki kutokana na uwezo wake.

Kuhusu kufanya nyimbo na Harmonize, Dimaond amesema kuwa hilo ni makubaliano ya wao wawili na kama likifanyika hakuna shida watafanya nyimbo ya pamoja.

Harmorapa ni mwanamuziki chipukikizi ambaye kwasasa anatamba na nyimbo yake inayokwenda kwa jina la ‘Kiboko ya Mabishoo’ aliyomshirikisha Juma Nature.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *