Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva, Tunda Man amesema kuwa kwasasa meneja wake Babu Tale ayupo karibu na Tip Top Connection kama zamani.

Tunda Man amesema ni ukweli usiopingika kuwa Babu Tale haithamini Tip Top kama siku za nyuma na ni kitendo ambacho kinamuumiza sana msanii huyo.

Pia Tunda Man amesema kitendo cha kutokuwa sawa na Babu Tale ni kitu anachokijutia sana kuwahi kumtokea kwa mwaka 2016.

Kauli hiyo ya Tunda Man inafuatia baada ya meneja huyo wa Tip Top kujikita zaidi katika kundi la WCB linaloongozwa na Diamond Platnum huku akilisahau kundi lake la zamani.

Katika mistari ya mwana hip hop nchini ROMA aliandika kuwa meneja kaikana Tip Top na kumganda Dangote kauli amabayo imetafsiliwa kama ni dongo kwa Babu Tale ambaye amekuwa karibu na Diamond ambaye ujiita Dangote na kuikacha Tip Top.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *