Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa reli mpya ambayo itatumika kupita treni za umeme ambapo awamu ya kwanza itaanza Dar es Salaam mpaka Morogoro itakamilika baada ya miezi 30.

Katika awamu hiyo ya kwanza reli hiyo inayotarajiwa kukamilika baada ya miezi 30 na itakuwa na urefu wa kilomita 300 ambapo kutakuwa na station sita huku treni ikitarajiwa kutumia muda wa masaa 2 na dakika 15.

Rais Magufuli amesema reli hiyo itakuwa na awamu tatu ambapo itakuwa urefu wa kilomita 1219 ikiwemo Dar es Salaam hadi Morogoro (Km 300), awamu ya pili ni Morogoro mpaka Makotopola (km 336 itagharimu kiasi cha dola milioni 1.22 ambayo ni sawa na shilingi trilioni 2.8 kwa fedha za Tanzania.

Ameendelea kuwa tayari serikali imeshalipa kiasi cha bilioni 300 wiki iliyopita ambapo bajeti yake ilitengwa tangu mwezi Julai mwaka jana.

Ameongeza kuwa treni hizo zitakazokuwa na spidi ya 160 zitapita kwenye reli hiyo na zitakuwa na uwezo wa kubeba tani 10,000 (sawa na malori 500 yenye uwezo wa kubeba tani 20 kila moja). Ajira takribani milioni moja zinatarajiwa kupatikana kupitia reli hiyo.

Magufuli amesisitiza kwa kusema baada ya nchi ya Uturuki kuona katika awamu ya kwenza Tanzania imegharamia ujenzi huo wa reli kwa fedha zake binafsi, imeamua kutoa mkopo wa nafuu kupitia mabenki yake matano katika ujenzi wa reli utako anzia Morogoro hadi Makotopola.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *