Mwanamuziki mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kanda Bongo Man ameomboleza kifo cha baba yake msanii wa Bongo Flava, Pam D, Shedrack Nyato kwa kutuma ujumbe kupitia whatsapp.

Nyato alikuwa mpiga gitaa la base kwenye bendi ya muimbaji huyo na walisafiri pamoja kutumbuiza kwenye nchi mbalimbali.

Bongo Man amemtumia ujumbe wa WhatsApp Pam D na kumuomba asome maneno aliyoandika kabla hajazikwa.

“Hey Festo jamaa yangu, tulisafiri wote Marekani, Canada, Zimbabwe, Visiwa vya Komoro, Mayotte, Reunion Island, Malawi na Australia. Hukuwa tu mwanamuziki bora niliyekutana naye katika maisha yangu lakini mmoja wa wanamuziki niliowachagua kutumbuiza pembeni yangu. Mungu akubariki na lala salama. Ujumbe toka kwa Bongo Man,”

Souce: Bongo 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *