Muigizaji nyota wa Bongo movie, Aunty Ezekiel amefunguka kwa kusema kuwa hana mimba nyingine kama watu wanavyosema kutokana na hali yake ilivyosasa.

Kauli hiyo ya Aunty inakuja kufuatia watu kueneza habari katika mitandao ya kijamii uhenda muingizaji huyo akawa na ujauzito kutokana na kujificha zaidi na hali yake kuwa tofauti na hapo awali.

Aunty hajaweka wazi kama ni kweli ni mjamzito ila alichokisema ni kuwa anatamani tena kupata mtoto mwingine wa kike baada ya mtoto wao wa kwanza Cookie naye kuwa wa kike.

Aunty Ezekiel ameongeza kuwa hataki kuweka wazi kama ni mjamzito kwa sasa ila watu watafahamu tu kwa kuwa hata mimba yake ya kwanza aliificha lakini watu waliweza kuibaini.

Muigizaji huyo ana mtoto mmoja aliyezaa na mwanaume wake mchezaji show wa Diamond, Moses Iyobo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *