Mwanamuziki mkongwe na Mbunge wa jimbo la Mikumi, Profesa Jay amemuandikia ujumbe wa kumpongeza mwanamuziki mwenzake Darassa anayefanya vizuri kwasasa kwenye anga ya muziki wa Bongo fleva.

Profesa Jay ametumia akaunti ya Instagram kuandika ujumbe huo wa kumtia moyo Darassa kutokana na nyimbo zake kuwabamba mashabiki wake.

Profesa Jay ameandika maneno haya

Mdogo wangu @darassacmg Imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya Usiku na Mchana ndio imekufanya ufikie hapo ulipofikia, Nakumbuka wakati unashoot Wimbo wako wa USIKATE TAMAA uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu, Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya JUA Ukiset GOALS, kufanya kazi kwa bidii na SALA yote Yanawezekana, Naamini kwa style hii ya JIWE juu Ya JIWE, NDOTO yako inakwenda kuwa kweli, Cha MSINGI usiridhike na mafanikio haya..HUU ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako at your DOOR, Keep your eyes open and Keep ya HEAD UP,
SKY IS THE LIMIT, GO GET DEM… BLESS
#ACHA MANENO WEKA MUZIKI
@darassacmg @darassacmg

Darassa kwasasa anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la ‘Muziki’ aliyemshirikisha Ben Pol na kumuwezesha kupata airtime kwenye vituo vya radio na TV mbali mbali mpaka kupelekea wmashabiki kuuita nyimbo hiyo kama wimbo wa taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *