Baada ya kusambaa video katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo inasemekana kumuhusu Paula ikimuonesha akifanya mapenzi na mtu mzima, mama mzazi wa binti huyo ambaye ni muigizaji wa Bongo movie, Kajala Masanja amekanusha uvumi huo.

Video hiyo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha binti mdogo wa chini ya miaka 18 akifanya mapenzi na mtu mzima ndani ya Gari.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Kajala Masanja amesema kuwa watu wanajua kabisa ile video iliyosambaa siyo binti yake bali wanapenda kumuaribia na huku akikanusha kumlea vibaya mtoto wake.

Muuigizaji huyo kupitia instagram ameandika:

Hey everyone….jamani mimi sina shida na mtu kama akinichukia au akinisema mimi kwa kitu chochote kile…kwasababu najua binadamu kuongea mmezoea..ila katika kuongea kwenu,kuingilia na kujudge my life naomba msimuingize mtoto wangu…sijawahi kumuomba mtu anisaidie kulea hata siku moja…mimi nimeona kuna video insambaa mnasema ni mwanangu na mnajua kabisa sie paula huyo ila ilimradi tu mfurahishe roho zenu…nilinyamaza…ila sasa naona mnakoelekea ni pabaya..mnahisi yeye hana moyo? Au mnahisi haumii?.mwanangu anasoma na sitaki mumchanganye na mambo yenu ya kipuuzi…vitu vibaya mnavyo muombea mwanangu viwarudie wenyewe…leave my daughter alone jamani…give us a break..fanyani tu mambo yenu yatakayofanya mpate faida katika maisha”,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *