Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwataka watu kuacha kumuandama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenye mitandao ya kijamii.

Wolper amewtaka watu kuacha kumwandama kwa kashfa ya kufoji vyeti pamoja na kumtukana katika mitandaoni jamii.

Kupitia akaunti yake hiyo Walper ameandika  “Nimevaa kiatu chake kimenibana mpaka kinataka kunipasua kisigino,”.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Jamani wa Tanzania tuwe na utu, acheni kumtukana huyu kaka daaaah hivi ni nani ambae yupo perfect mpk aanze kumtukana kaka wa watu jmn. Nimepost nikiwa km binadam wa kawaida ambae nina moyo!muhurumieni kaka watu acheni Mungu awe muhukumu basi,”.

Muigizaji huyo ameamua kuandika maneno hayo kutokana na baadhi ya watu kumuandama mkuu wa mkoa huyo kuhusu elimu yake pamona na kashfa nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *