Mkali wa ngoma ‘Dume Suruali’ Mwana FA amemwagia sifa aliyekuwa meneja wake wa zamani Boniventure Kilosa ‘DJ Bony Love’ baada ya kushinda tuzo ya heshima kwenye tuzo za EATV Awards zilizofanyika jana Mlimani City.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram FA amesema kuwa DJ huyo ndiyo aliyemfanya aingie kwenye muziki baada ya kumuamini na kuanza kufanya nae kazi.

Kupitia akaunti yake ya Instagram FA ameandika kama ifuatavyo   “Sidhani kama ningefanya mziki kama sio Boni..brother ndio alikuwa mtu wa kwanza kwenye industry kuniamini na kunipa nafasi..i cant thank you enough mzazi,EVER..nimefarijika mno..asante sana EATV kwa kumpa tuzo ya heshima,ambayo ni stahili yake @boniluv ..hongera sana mzazi! Pia hongera nyingi kwa EATV kwa kufanikisha hili zoezi la tuzo..hongereni kwa hii platform na kiukweli haikukaa kama ndio mara ya kwanza kwa jinsi mlivyoipatia..hatua kuelekea kwenye right direction,MMETISHA SANA” – Mwana FA

Mwana FA alikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wanawania tuzo hizo kwenye kipengele cha mwanamuziki bora wa mwaka ambapo Alikiba aliibuka mshindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *