Mkali wa ‘Marry You’ Diamond Platnumz ameifariji familia ya mwanamuziki wa hip hop nchini Roma baada ya kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa stidio za Tongwe jijini Dar es Salaam juzi usiku.

Kupitia akaunti yake Instagram Diamond ameonesha kuguswa na tukio hilo lililosisimua watu wengi nchini kutokana na kutekwa kwa mwanamuziki hao.

Diamond ameandika kama ifuatavyo

Wakati mwingine natafakari sijui hata wapi tunaelekea… lla kwakuwa Mwenyezi Mungu ndio Mpangaji wa yote basi naamini hata hili litapita tu”.

Pia ameongeza “Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya @roma2030 na wanamziki wenzetu wote ambao hadi sasa haijajulikana walipo”.

Roma na wenzake watatu wamekamatwa usiku wa juzi katika studio za Tongwe zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam ambazo zinamilikiwa na J-Murder.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *