Baada ya kwenda Nairobi kumjulia hali Tundu Lissu aliyepigwa risasi, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa waliomshambulia Lissu wamemuumiza sana.

Zitto Kabwe ameeleza hayo kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii baada ya kurejea nchini akitokea Nairobi nchini Kenya.

Zitto ameandika kama ifuatavyo

Ujasiri ni nini ?
Zitto Kabwe
Nimetumia wikiendi iliyopita kumsabahi ndugu Tundu Lissu jijini Nairobi. Nimerudi nikiwa mwenye unyenyekevu zaidi kwasababu ya nguvu na ujasiri ambao kaka yangu ameuonyesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali.
Si mara nyingi hapa nchini utasikia tukiongelea ujasiri. Lakini namfikiria Lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi. Najua hivyo ndivyo alivyo. Waliomshambulia wamemuumiza. Wamemuumiza kweli. Na bado wakati tuliokuwa naye amenionyesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri.
Alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu sio kitu rahisi kwa mtu yoyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha nimeumia moyo Sana kama asingesema maneno haya kwangu “tumeshinda. Tumeshashinda”.
Ujasiri ni Lissu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *