Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa hakwenda Nairobi kumuona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwasababu asingeweza kumuona akiwa kwenye maumivu.

Wema ameweka wazi maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni baada ya dakika chache tangu kuachiwa kwa picha za kwanza za Mbunge huyo akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Wema ameanza kwa kuandika “Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvuz zaidi….Utarudi tena ukiwa na nguvu kuliko ulivyokuwa awali…Shujaa wetu. … Picha hii imenifanya nipate hisia.

Pia ameongeza kwa kuandika ‘Sasa naweza andaa safari ya Nairobi kuja kukuona.. Awali nisingeweza kuvumilia kukuona ukiwa kwenye maumivu”.

Wema Sepetu ametajwa na Chama cha  Chadema kama mmoja wa wahamasishaji  aliyeweza kuhamasisha watu kutoa michango kwa ajili ya matibabu ya Mbunge Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa kwenye gari lake nje ya makazi yuke huko mjini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *