Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amewataka watu kutokata tamaa katika maisha kwani hata yeye hakufikiria kuishi Maisha mazuri anayoishi kwasasa.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Shilole ameanza kwa kuandika ‘Nikiwa hivi sikuwa naijua kesho yangu Sikuwahi jua nitakuwa shishi wa leo mwenye shishi food, mwenye watu wengi nyuma yangu, mwenye uthubutu wa mengi sana na mchango katika jamii na serikali yangu.

Nilikuwa nina tumaini tu kuwa siku moja mambo yatakuwa sawa
Nikiiangalia leo yangu nabaki namshangaa sana Mungu
Alhambdulillah kwa kila kitu.

Kama kuna mtu amekata tamaa hana tumaini basi asimame afute vumbi asonge mbele, kila kitu kinawezekana Ukijipa muda wa subra na kupambana.

Pia amesema kuwa MUNGU AKISEMA NDIO HAIJALISHI WEWE NI NANI AU UNAPITA WAPI ILA HAKUNA WA KUSEMA HAPANA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *