Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amefunguka na kuwachana wanawake kwa kusema kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Shamsa Ford ameandika maneno ambayo yanamlenga mzazi mweza na Diamond, Hamisa Mobeto.

Ameanza kwa kuandika “Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie.haitakuja kutokea kamwe wanawake tukapendana.mwanamke ndo huwa mstari wa mbele kumuumiza na kumdhalilisha mwanamke mwenzie.kabla ya kumuumiza mwanamke mwenzio jaribu kuvaa viatu vyake ingekuwa wewe ungefanyaje..wanawake sisi daaa####TUNAHITAJI MAOMBI

Shamsa amekuwa akiutumia ukurasa wake wa instagram kuandika mambo mbalimbali ya kushauri wanawake na watu ambao bado hawajaingia kwenye ndoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *