Muigizaji wa Bongo Movie, Riyama Ally  amewashambulia wezi wa mtandaoni wanaofanya shughuli za kuiba akaunti za watu maarufu nchini.

Riyama amefunguka hayo baada ya akaunti ya mumewe kuibiwa na watu wasiojulika na kuitangaza kuiuza.

Muigizaji huyo amesema kuwa wezi hao wameichukua akaunti  ya mumewe na kufuta picha zote kisha kutangaza kuiuza kwa Sh. 70,000.

riyama-2

Riyama ameeleza kuwa mwizi huyo ameshapatikana na watamchukulia hatua za kisheria ili liwe fundisho kwa wezi na matapeli wengine wa mtandaoni.

Wizi wa akaunti za watu maarufu umekuwa mkubwa sana hapa nchini na duniani kwa ujumla ambapo hivi karibuni waliiba akaunti ya mwanamuziki, Harmorapa na kuanza kutukana baadhi ya wasanii akiwemo Diamond.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *